Zahera ageukia madai ya ushirikina Yanga
0
November 04, 2019
Kocha Mkuu wa Yanga, Mwinyi Zahera ameibuka na kutoa ufafanuzi kuhusiana na baadhi ya madai ya wachezaji wake kujihusisha na ushirikina.
Akiongea na moja ya gazeti nchini, Zahera ametoa ufafanuzi huo kufuatia kuwepo kwa tetesi kuwa ushirikina umekuwa ukichukua nafasi ndani ya kikosi kwa baadhi ya wachezaji.
Kocha huyo alisema hayo alipoulizwa kuhusu suala la madai ya wachezaji kukimbia kucheza nafasi ya Juma Abdul kwa kuwa wanaumia wakihusisha na ushirirkina.
“Ni kweli alicheza Mapinduzi aliumia lakini sikuweza kumtumia Juma Abdul kwa kuwa alichelewa kwenye maandalizi ya msimu kutokana na matatizo yake na uongozi akiwa na Dante.
“Sasa wakati anakuja Morogoro sisi tulikuwa tumeshamaliza maandalizi yeye ndiyo akawa amekuja lakini hakuwa anacheza kwa kuwa hakuwa fiti kabisa tofauti na wenzake lakini tulivyokuwa Mwanza ambapo nilipanga kuanza kumtumia ndiyo akapatwa na msiba wa mama yake, akaondoka.
“Kukamilisha idadi lakini siyo kucheza kwa kuwa bado hakuwa sawa na siyo kweli kwamba wachezaji walikuwa wakiogopa kucheza kwenye nafasi hiyo,” amemalizia Zahera.
Ikumbukwe Yanga wamekosa nafasi ya kuingia kwenye hatua ya makundi katika michuano ya kombe la shirikisho kwa kufungwa na Pyramids fc kwa mabao 3-0 katika mchezo wa marudiano uliopigwa jana usiku nchini Misri huku mchezo wa awali uliisha kwa kwa Yanga kufungwa mabao 2-1 kwenye dimba la CCM Kirumba jijini Mwanza.
Tags