Waugua Ugonjwa wa Kuhara BAADA ya Kula Chakula Msibani....



Watu 37 wanatajwa kula Chakula chenye sumu walipokuwa msibani katika eneo la Mtumba jijini Dodoma, ambapo wote wameshafikishwa katika Hospitali ya Mkoa wa Dodoma na wanaendelea na matibabu

Mganga Mkuu wa Hospitali ya Dodoma Dkt. Ibenzia Ernest amethibitisha hayo wakati akizungumza na vyombo vya habari ambapo tayari timu imeshaenda kwa ajili ya uchunguzi.

"Ni kweli tumepokea watu 37, na tunaendelea na matibabu na walikula hicho chakula jana jioni, na walikula ugali maharage, na uzuri zaidi hakuna taarifa ya kifo." amesema Mganga wa Hospitali ya Dodoma "Tumeshatuma wataalam ndani ya muda mfupi mtapata majibu." ameongeza Dkt. Ernest
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad