Achoma Nyumba ya MKE Mweza Kisa Pesa ya Christmas


Mwanamke mmoja nchini Kenya, anayejulikana kwa jina la Anne Sande, anashikiliwa na Polisi baada ya kuchoma moto nyumba ya Mke mwenzake siku ya Alhamisi Disemba 19.



Mwanamke huyo amechoma moto nyumba hiyo kwa hasira, baada ya Mumewe Dominic Miti kumpa mke mwenzie pesa za Kenya Ksh 1000, za sikukuu ya Christmas huku yeye akiachwa mtupu .

Akizungumza na chombo kimoja cha habari nchini humo Mume wa wanawake hao Dominic Miti amesema, alijaribu kumsihi Mkewe awe mtulivu na kumpa siku kadhaa za kutafuta hela za kumnunulia bidhaa za sikukuu, lakini mkewe hakusikia.

"Nilikuwa napanga kumpa KSh 1,000. Hata hivyo hakutaka kuwa mtulivu" amesema Dominic Miti

Mwanaume huyo na mkewe walikamatwa na kufikishwa katika Kituo cha Polisi, lakini mume huyo aliachiwa siku moja.

Source, Tuko News

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad