MTANDAO maarufu duniani wa WhatsApp hautafanya kazi kwenye simu janja zinazotumia mfumo wa Window ‘Window Smartphone’ kuanzia leo Desemba 31, 2019, kwa mujibu wa mtandao wa Mirror.
Mtandao huo unaotumiwa na mabilioni ya watu hivi sasa, umesema umeamua kuondoa huduma hiyo kwenye simu janja za makampuni mengine.
Simu zitakazoathirika katika miezi ya hivi karibuni ni pamoja na baadhi ya simu janja za Android pamoja na baadhi za iPhone.
Simu za Android toleo la 2.3.7 hazitakuwa na uwezo wa kutengeneza akaunti mpya au kuboresha (update) akaunti zao za zamani ifikapo Februari 1, 2020.
Pia simu za iPhone zinazofanya kazi kwenye mfumo wa iOS 8 pia hazitaweza kutengeneza akaunti mpya au kusitisha akaunti zao za zamani ifikapo tarehe hiyo.
“Hautakuwa na uwezo wa kutumia WhatsApp kwenye simu janja zinazotumia mfumo wa Window baada ya Desemba 31, 2019, pia WhatsApp inaweza isipatikane kwenye ‘Microsoft app store”, ulisema uongozi wa mtandao huo.