Amenipiga Amening'oa Nywele ANATAKA Turudiane Anasema Amebadilika


Habari Kaka Iddi, samahani sikukutafuta mapema kwakua nilikua nimelazwa hospuiitalini, mimi ni yule dada nilikupigia kipindi flani kuhusu mchumba wangu ambaye kila nikimfumania alikua ananipiga na kuniambia kua nilikua namdhalilisha kwa kumfumania na kumfuatilia.

Nilikueleza mambo mengi namna alivyokua ananipiga bila kujali kua ni mjamzito. Najuta kwani sikukusikiliza uliponiambia niondoke, mara ya mwisho alinipiga na kunifungi nnje usiku mzima ndiyo ukaniabia asubuhi akifungua mlango nichukue kilichochangu niondoke. Nilichukua kweli nakurudi kwetu lakini baada ya wiki mbili alianza kunitafuta akatuma watu.

Ndugu zake walikuja na kunishawishi akaniambia anataka kunioa, alipoongea kuhusu ndoa na namna alivyokua anasema niliamua kumpa nafasi nyingine kwani nilikua na mimba yake, tukafunga ndoa ya Msikitini. Mwezo wa kwanza wa ndoa ulikua mzuri lakini alibadilika tena na kuanza kunipiga na kila nikigusa simu yake, Dada yangu aliniambia nisiguse ila wewe uliniambia tatizo si simu ni yeye hivyo nisiondoke.

Niliacha kushika simu kweli lakini sikuweza kuondoka niliendelea kuvumilia, nakuandikia kwakua juzi amenipiga, mpaka mimba kutoka ilikua ya miezi nane hivyo mtoto kafia tumboni na katoka mzima, nilienda saluni nikachelwawa kurudi, kashika rasta nilizosukia kavuta mpaka kaning’oa nywele, hapa nilipo ni makovu matupu. Baada ya kunipiga na kuona nimeumia sana aliondoka hata kazini hayupo.

Sijui yuko wapi ila ananitumia meseji na kunipigia simu nimsamehe anadai kua kajifunza kwani kumpoteza mtoto kumemchanganya sana, anadai ni pepo ndiyo limfamfanya anipige. Nimechanganyikiwa sijui chakufanya, nyumbani wananiambia niondoke lakini mimi bado nampenda na nahisi safari hii atabadilika kwani anaonekana kujutia kweli, niko njia panda sijui hata nifanye nini?
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad