Ashikiliwa na POLISI Kwa Kumlazimisha Mtoto wa Miaka Miwili Kunywa Bia

Polisi nchini Kenya wanamshikilia Mwanaume wa miaka 30 kwa tuhuma za kumlazimisha Mtoto wa miaka 2 kunywa bia wakati wa Siku Kuu ya Krismasi.

Baada ya tukio hilo, Wanafamilia walimkimbiza Mtoto huyo Hospitali wakihofia kuwa Mtoto huyo anaweza kupoteza maisha.

Wanakijiji waliandamana hadi Kituo cha Polisi kutoa taarifa ya tukio hilo na kusaidia kukamatwa kwa Mercus Kinyua ambaye anatuhumiwa kwa kumnywesha bia Mtoto huyo.

Polisi wameonya tabia hiyo na kuongeza kuwa hali ya Mtoto ilikuwa mbaya kwani tayari kiywaji hicho kilimlevya.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad