Athari za Mvua..Huduma za Mwendokasi KUPITIA Jangwani Zasitishwa


Kutokana na mvua inayoendelea kunyesha katika Mkoa wa Dar na kusababisha sehemu mbalimbali kujaa maji, Wakala wa Mabasi Yaendayo Haraka (DART) imesitisha huduma za mabasi hayo katika njia ipotayo Jangwani eneo la Mto Msimbazi

DART imewashauri wasafiri kutumia usafiri mbadala wafikapo Kituo Kikuu cha Morocco ili kufika Mjini Kati au Kariakoo, na kwa wanaotoka Mjini Kati au Kariakoo wanashauriwa kutumia usafiri mbadala hadi Morocco ambapo wanaweza kuendelea kupata mabasi ya DART

Aidha, imeainisha kuwa, licha ya kutokea mafuriko Jangwani, huduma ya Mabasi ya Mwendokasi inaendelea katika njia za Kimara hadi Magomeni Mapipa, Kimara hadi Morocco na Gerezani hadi Muhimbili

Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad