Boeing Kuacha Kuzalisha Kwa Muda Ndege za 737 Max Kuanzia January 2020



Kampuni ya Boeing imetangaza kuwa itasimamisha kwa muda uzalishaji wa ndege zake zilizokumbwa na matatizo za 737 Max kuanzia Januari 2020

Utengenezaji wa ndege hizo ulikuwa ukiendelea licha ya ndege hizo kuzuiwa kupaa kwa mezi 9 sasa baada ya kuhusika katika ajali mbili zilizosababisha vifo vya mamia ya watu.

Zaidi ya watu 300 walipoteza maisha wakati ndege mbili za 737 Max zilipoanguka nchini Indonesia na Ethiopia baada ya kuripoti matatizo katika mfumo wake mpya

Boeing ilikua ikitumaini kuwa ndege hizo zitarejea tena angani kufikia mwishoni mwa mwaka huu lakini wasimamizi wa safari za anga nchini Marekani wamesema ndege hizo hazitapewa kibali cha kurejea angani katika siku za hivi karibuni

Kampuni hiyo imesema katika taarifa yake kwamba haitawafuta kazi wafanyakazi waliopo wa 737 Max, lakini kusimamishwa kwa utengenezaji kunaweza kuwaathiri wasambazaji na uchumi kwa ujumla 

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad