Boris Johnson Aapishwa Rasmi kuwa Waziri Mkuu wa Uingereza



Kiongozi wa Chama cha Kihafidhina cha Uingereza Bw. Boris Johnson jana aliapishwa rasmi kuwa waziri mkuu wa Uingereza baada ya kushinda kwenye uchaguzi wa Baraza la chini la bunge la Uingereza.

Kwenye hotuba aliyotoa jana baada ya ushindi Bw. Johnson alisema Uingereza imetandika njia na kumaliza mvutano na kukaribisha zama mpya. Amesisitiza kuwa Uingereza itajitoa rasmi kwenye Umoja wa Ulaya tarehe 31 mwezi ujao.

Wakati huohuo, mkutano wa kilele wa siku mbili wa Umoja wa Ulaya ulikamilika jana mjini Brussels, ambapo viongozi wa umoja huo walijadili juu ya masuala ya Brexit, Makubaliano ya Umoja wa Ulaya ya kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi, na mageuzi ya Shirika la Biashara Duniani. Pia wamehimiza Uingereza kuidhinisha na kutekeleza makubaliano ya Brexit haraka iwezekanavyo.
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad