Bosi wa TRC ajibu Ushindani wa usafiri wa Treni na Mabasi



Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Reli Tanzania (TRC), Masanja Kadogosa ameeleza juu ya dhana potofu watu kuzungumzia kwamba usafiri wa Treni una ushindani na usafiri wa Mabasi.

Kadogosa amesema kuwa Wamiliki wa Mabasi na Malori wanatakiwa kuangalia namna ya kutumia fursa hiyo kwa ajili ya kutanua Wigo wa huduma wanazozitoa.

“Kuna dhana potofu kwamba Usafiri wa Treni una Ushindani na Usafiri wa basi, lakini hiyo sio sahihi, badala yake Wamiliki wa Mabasi na Malori wanatakiwa kuangalia namna ya kutumia fursa hiyo kwa ajili ya kutanua Wigo wa huduma wanazozitoa, ikiwa ni pamoja na kuanzisha safari za kutoka katika Vituo vyetu Vikuu kwenda katika maeneo ambayo hatuyafikii, "amesema Masanja Kadogosa katika kipindi cha Clouds 360.

Hata hivyo Kadogosa aliongeza kuwa “Usalama kwenye Treni ni Kipaumbele chetu cha kwanza, usalama ndani ya treni yetu ni mkubwa sana kwani kuna Kikosi cha Polisi cha reli ambacho kinahakikisha usalama wa Treni pamoja na Abiria na mali zao, hivyo hakuna sababu ya Watu kuhofia usalama wao katika safari za treni.”

Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad