Breaking: Tito Magoti Achukuliwa na Watu Wasiojulikana



 MFANYAKAZI wa Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu (LHRC), Tito Magoti,  anadaiwa kachukuliwa na watu wasiojulikana akiwa maeneo Mwenge, jijini Dar es Salaam muda mfupi uliyopita.

Inadaiwa  amechukuliwa na watu watano waliovalia kiraia ambao wanadaiwa kumfunga pingu kabla ya kuondoka naye kusikojulikana wakiwa na gari aina ya Harrier.

Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu, kupitia akaunti yake ya Twitter kimethibitisha tukio hilo na kuandika: “Tumepokea taarifa za kuhuzunisha kwamba Afisa wetu wa Kitengo cha Elimu kwa Umma, Bw. Tito Magoti ametekwa na watu waliovalia mavazi ya kiraia maeneo ya Mwenge, jijini Dar es Salaam. Tunaendelea kufuatilia taarifa hizo na tutatoa taarifa zaidi. #BringBackTito.”
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad