Carlo Ancelotti na EVERTON Wafikia Makubaliano ya Awali...



Kwa mujibu wa Shirika la Habari la Sky Sports, Carlo Ancelotti na Klabu ya Everton wamefikia makubaliano ya awali ya Kocha huyo kuinoa timu hiyo yenye makazi yake huko Merseyside

Majadiliano hayo yanaelezwa kufanyika baada ya Ancelotti kuwasili Merseyside jana huku ikidaiwa kuwa atatangazwa kabla ya mchezo wa robo fainali wa Jumatano kwenye Michuano ya Carabao ambapo Everton inavaana na Leicester City

Ancelotti, aliyefutwa kazi na Klabu ya Napoli wiki iliyopita, amewahi kuifundisha Klabu ya Chelsea ya England (2009-2011) na kufanikiwa kuchukua Kombe la Ligi Kuu England, Kombe la FA na Ngao ya Jamii lakini katika Ukocha wake amechukua makombe Matatu ya Klabu Bingwa Ulaya
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad