Chato Waanza Kutekeleza Agizo la Rais Magufuli
0
December 08, 2019
Geita. Halmashauri ya Wilaya ya Chato mkoani Geita nchini Tanzania imeanza kutekeleza agizo la Rais wa nchi hiyo, John Magufuli alilolitoa la kutaka ujenzi wa upanuzi wa Hospitali ya wilaya hiyo kuanza mara moja.
Jana Ijumaa Desemba 6, 2019 akiwa hospitalini hapo Rais Magufuli aliwataka viongozi wa halmashauri hiyo kuacha kupoteza muda mwingi wakibishana juu ya upanuzi huo na kumtaka Waziri wa Tamisemi, Seleima Jaffo na mkurugenzi wa halmashauri hiyo, Eliud Mwaiteleke kuhakikisha ujenzi unafanyika kwa gharama zinazostahili.
Kufuatia agizo hilo, Mwaiteleke kwa kushirikiana na Mganga Mfawidhi wa Hospitali hiyo, Dk Ligobeth Kalisa leo Jumamosi Desemba 7, 2019 wameanza kusimamia ujenzi wa hospitali hiyo unaotarajiwa kukamilika ndani ya kipindi cha miezi minne.
Katika taarifa iliyotolewa na ofisa habari wa halmashauri hiyo, Richard Bagolele imeeleza ujenzi wa upanuzi wa hospitali hiyo utahusisha ujenzi wa jengo la wagonjwa wa nje, maabara, jengo la baba, mama na mtoto, jengo la wazazi pamoja na sehemu ya kuchomea taka ambayo yote kwa pamoja yatagharimu Sh1 bilioni.
Tags