Mkuu wa wilaya ya Makete mkoani Njombe Veronica Kessy ameagiza wananchi wilayani humo wanaodaiwa na vyama vya ushirika kuhakikisha wanarejesha madeni yao kabla ya muda uliopangwa ili kuepusha kuepusha kuuziwa mali zao.
Mkuu wa wilaya hiyo ametoa agizo hilo hii leo katika kikao cha wanamakete wazawa wanaoishi ndani ya wilaya ya Makete na nje ya wilaya na kilichoandaliwa na chama cha maendeleo Makete (M.D.A) na kufanyika katika ukumbi wa madihani wilayani humo.
“Nafahamu wanamakete mmekuja nyumbani kuna ndugu zenu ambao wanahusika,maana yake wanafuatiliwa mpaka wadhamini ambao walisimamia mikopo hiyo kuchukiliwa kwenye vyama,msaidie na ninyi mliokuja ndugu zenu waliokopa fedha hizo ziludi hakuna salia mtume hata kama mtu ni marehemu,yupo aliyemuandika kama mrithi lakini wakumdhamini na mali zile zitachukuliwa”alisema Veronica Kessy
Amesema wilaya ya Makete kupitia vyama vya ushirika fedha ambazo zimekopwa na zipo nje huku bado hazijarejeshwa, ni milioni mia nne hamsini na sita na laki tisa.
“Kwa hiyo tathmini iliyofanyika kwa mkoa wa Njombe fedha zinazodaiwa kwa wanachama kwenye Amcos na Saccos ni bilioni 6.6 na zile tarehe alizokuwa ametoa mkuu wa mkoa 24 mpaka tarehe 11 disemba ilikuwa imeludishwa milioni mia tatu tu,kwa hiyo tumeagizwa wakuu wa wilaya tusimamie tuhakikishe kiasi cha shilingi bilioni 5.7 kinarejeshwa haraka sana na imetolewa mpaka tarehe ishirini na moja mwezi wa kwanza fedha hizo ziwe zimerudi”alisema DC Kessy
Aidha amewaagiza wanamakete kujipanga kikamilifu kuyafikia mafanikio kutokana na ujenzi wa barabara kwa kiwango cha lami wilayani humo.
“Tunathamini sana michango mnayoifanya mkiwa nje ya Makete na tunashuhudia kuona maendeleo makubwa ambayo mnayafanya huko nje,sasa tunahitaji hayo maendeleo yaludi nyumbani,tunamaliza mwaka 2019 tunaingia mwaka 2020,tuwe na malengo ya muda mfupi,muda wa kati na muda mrefu”aliongeza Veronica Kessy.