Diamond Awajibu Waliomshambulia Kwenye Tamasha la Ecofest



Baada ya jana kuibuka gumzo la kumshambulia msanii wa Bongofleva nchini Tanzania, Diamond Platnumz kutokana na mameneja wake kuonyesha kuwa amejaza watu kwenye shoo ya Ecofest iliyofanyika nchini Sierra Leone, mwenyewe awajibu.

Diamond alianza kushambuliwa mitandaoni baada ya meneja wake, Babu Tale alipoonyesha picha ya mashabiki wakiwa wamejaa uwanjani nchini Sierra Leone na kusindikizwa na maneno na kueleza kuwa : “Mimi nikisemaga naonekana mswahili ila siachi kusema atutaki mumfananishe Diamond Platnumz na mpuuzi yoyote. Hii ni Freetown Sierra Leone muda wao saizi ndio kwanza saa tano uwanja umejaa, wanamsubiria mtoto wa Tandale .

Baada ya watu kuona video na maneno hayo, walimshambulia Tale na kusema  tamasha hilo linashirikisha wasanii wengi, lakini wao wamelifanya kama ni la Diamond.

Jana Jumapili Desemba 1, 2019 kupitia ukurasa wake kwenye mtandao wa Instagram, Diamond aliandika, “Kuna baadhi ya Watanzania wamezaliwa kuchukia, wakiona Watanzania wenzao wanafanikiwa na kuipa sifa nchi hao niachieni mimi, nitadeal nao na safari hii watashusha viingilio mpaka viwe shilingi mia !!.

Diamond anaungwa mkono na msanii Nahreel anyeunda kundi la Navykenzo, ambaye naye aliandika’ Ingekua ni msanii ambae sio Mtanzania hapo, ungesikia wasanii wa bongo mnakwama wapi? ila kafanya Diamond Platnumz basi its a different story, juzi mwakinyo (boxer) kashinda tunasema kabebwa.

“Samatta asipoifungia taifa mnasema sio mzalendo, Watanzania sisi sijui ni watu wa aina gani, ndio maana hata juzi kilichotokea kwenye tamasha la msanii wa nje wasanii wa ndani tukanyamaza ,tujivunie.

Tamasha hilo linajulikana kwa jina la Ecofest

linalojumuisha nchi za  Jumuiya ya kiuchumi ya nchi za Afrika Magharibu lilifanyika katika Uwanja wa Taifa wa Free Town nchini humo Novemba 30, 2019, ambapo wasanii zaidi ya 15 kutoka nchi mbalimbali walialikwa na kutumbuiza

Hata hivyo Diamond alionekana kuwa kivutio kuanzia mapokezi yake hadi siku aliyopanda jukwaani kwa watu kutoogopa mitutu ya bunduki ya wanajeshi waliokuwa wakimlinda wakati anatumbuiza na kwenda kumkumbatia.

Kama vile haitoshi sio yeye Diamond wala viongozi wake, walitumia mitandao ya kijamii vilivyo katika kuonyesha hali ilivyokuwa kwa msanii huyo anayetamba na vibai 'Baba Lao' na 'Sound' na anayefanya vizuri ndani na nje ya nchi.
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad