'Ebitoke Ukitaka Msaada wa KUPIGANA Njoo Kwangu' - Shishi


Msanii na mfanyabiashara Zuwena Mohammed "Shilole" amesema ana uwezo wa kupigana kuliko mchekeshaji Ebitoke, na ikitokea kama Ebitoke anashida yoyote ya kupigana na mtu basi Shilole yupo tayari  kujitolea kupigana.

Shilole amesema wakati anatambumbilisha wasanii ambao wamejitokeza kwenye "Birthday Party" wakati anatimiza umri wa miaka 32 siku ya Disemba 20,

"Nimefurahi kumuona mdogo wangu Linah, Recho nawapenda sana vilevile mdogo wangu Ebitoke usiogope mimi napigana kuliko wewe, lakini usijali ukiwa na shida yoyote yakupigana wewe njoo uniambie, usinikodi nitaenda bure kwa kujitolea na napiga kuliko kikosi chochote maana mimi mwenyewe ni kikosi tosha"  ameeleza Shilole

Aidha ameongeza kuwa anashukuru sana watu wote waliojitokeza kufika kwenye siku yake hiyo muhimu wakiwemo wasanii, mashabiki zake pamoja na vyombo vyote vya habari. 

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad