Waziri Mkuu wa Mstaafu, Edward Lowassa amepongeza juhudi zinazofanywa na Serikali pamoja na Taasisi za dini kutatua migogoro ya wakulima na wafugaji mkoani Morogoro.
Alisema hayo, wakati wa ibaada maalumu ya shukrani ya Askofu Jacob Mameo Ole Paulo wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT) Jimbo la Morogoro ya kutimiza miaka 25 ya ndoa na 25 ya uchungaji.
Ibada iliyofanyika Usharika wa Bungo, Morogoro mjini, iliongozwa na Askofu Mkuu wa KKKT, Askofu Dk. Fredrick Shoo.
“Zamani ilikuwa ukifungua vyombo vya habari, unasikia migogoro ya wafugaji na wakulima Morogoro.
“Sasa hali ni shwari, ninawaomba viongozi na waumini wote tuendelee kuuombea mkoa huu uzidi kuwa na Amani na mshikamano,” alisema.
Ibada hiyo, iliudhuriwa na viongozi mbalimbali wa Serikali na kidini mkoani humo.