EXCLUSIVE : 'Haji Manara Hajielewi' - Alikiba
0
December 25, 2019
Mfalme wa BongoFleva Alikiba amesema, Msemaji wa Klabu ya Simba, Haji Manara, alikuwa hajielewi wakati aliposema Alikiba lazima aimbe kwenye siku ya harusi yake.
Alikiba amesema hayo kupitia EATV & EA Radio Digital, wakati alipoulizwa kuwa unatoa ahadi gani baada ya Haji Manara kusema lazima uimbe kwenye harusi yake, na asipoimba au asipotokea kwenye harusi hiyo basi hata akifa usiende.
Alikiba amejibu kuwa "aliliongea hilo suala akiwa hajielewi kiukweli, kwanza unajua katika Harusi kukitokea vitu kama hivyo hata Ndoa yako yenyewe inakuwa inakwenda kimuziki muziki tu, yeye alikuwa Mwalimu wangu wa Chuo cha Dini, kwa hiyo aite watu wa Madrasa wapige Ubwabwa na Maulid, mimi mwenyewe nitapiga Dufu"
Aidha Mfalme huyo wa BongoFleva ameongeza kusema "lakini akitaka alete mambo yake ya watu kwenda kuimba haifai au twende Kidini kama alivyokuwa akinifundisha mimi chuoni basi hata yeye apate matokeo yake pale"
Pia Msemaji huyo wa Klabu ya Simba, Haji Manara ametangaza kufunga Ndoa ifikapo mwaka 2020, ila hawezi kusema itakuwa lini kwa sababu anaogopa watu watamroga.
Tags