FAHAMU: Kijiji cha Wauza Figo ‘Kidney Village’


Leo June 19, 2018 kuna hii ya kuifahamu kuhusu Kijiji cha Hokse nchini Nepal kimebatizwa jina jipya la ‘Kidney Village’ baada ya Watu karibia wote wanaoishi kwenye kijiji hicho kuwa wameuza Figo zao.

Inadaiwa kuwa Wakazi wa Kijiji hicho hali zao za kiuchumi ni duni sana kitu kinachowasukuma kuingia katika biashara ya kuuza Figo zao ili wapate fedha za kujikimu mahitaji yao.

Mkazi mmoja aliyetambulika kwa jina la Geeta mwenye miaka 37 alisema kuwa yeye na Mume wake walisafiri mpaka kwenye Hospitali moja huko nchini India ili kutolewa Figo zao na kulipwa  zaidi ya shilingi Milioni 3 za Kitanzania.

Aidha familia hiyo ilitumia fedha hizo kununua kiwanja na kujenga nyumba yao na isivyo bahati nyumba hiyo iliangushwa na tetemeko la ardhi lililotokea kijijini hapo.

Kwa upande mwingine madalali wanaofanya biashara hiyo ya figo wametajwa kuzunguka sana katika kijiji hicho na kuwashawishi Wanakijiji hao kuuza Figo zao.

Millard

Top Post Ad

Below Post Ad