Familia Yenye Nguvu zaidi Ufilipino Yahukumiwa Kwa Mauaji
0
December 19, 2019
Mahakama nchini Ufilipino imewahukumu wanachama kadhaa wa ukoo ulio na ushawishi mkubwa wa kisiasa, kwa makosa 57 ya mauaji ya miaka 10 iliyopita yanayohusiana na uchaguzi.
Jaji Jocelyn Solis Reyes amewahukumu kifungo cha maisha au miaka 40 jela bila msamaha jumla ya watuhumiwa 27 kwa kukutwa na hatia ya kushiriki katika mauaji hayo.
Watuhumiwa wengine 15 walitiwa hatiani kwa kuwa washiriki wakati wa mauaji hayo na kuhukumiwa kifungo cha miaka sita jela, huku washitakiwa wengine zaidi ya 50 wakiachiliwa huru.
Mauaji ya mnamo Novemba 23 mwaka 2009 katika jimbo la Maguindanao kusini mwa mji mkuu, Manila, yalizusha hasira nchini Ufilipino na kimataifa, na yalimulika kukosekana kwa uwajibishwaji wa kisheria nchini humo. Watu 58 waliuawa wakati wa mauaji hayo.
Tags