Wakili wa kujitegemea, Fatma Karume, amesema kipi cha ajabu kwa Waziri Mkuu Mstaafu, Frederick Sumaye kuondoka Chadema wakati alishawahi kuhama CCM.
Fatma aliandika ujumbe huo kupitia ukurasa wake wa Twitter kuwa Sumaye alishawahi kuondoka CCM kwa kutokuchaguliwa kugombea Urais.
“Jamani mbona tunasahau haraka. Sumaye katoka CCM baada ya kutokuchaguliwa kuwa mgombea Urais 2015. Sasa kuna ajabu gani Sumaye kutoka Chadema baada ya kutokuchaguliwa kuwa mwenyekiti?
Aliongezea kuwa:” Can we please move on? Maana kuna mambo mengine ya Discuss ni kukimbia kwenye pipa huku huendi popote,” alisema
Leo Sumaye alitangaza kukihama cha cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) baada ya kudai alifanyiwa figisu katika uchaguzi ili asishinde nafasi aliyokuwa anaigombea.
Jamani mbona tunasahau haraka. Sumaye katoka CCM baada kutokuchaguliwa kuwa mgombea wa urais 2015. Sasa kuna ajabu gani Sumaye kutoka CDM baada kutokuchaguliwa kuwa Mwenyekiti? Can we please move on? Maana kuna mambo mengine kuyaDISCUSS ni kukimbia kwenye pipa huku huendi popote. pic.twitter.com/NHZ8Zx8ktj
— fatma karume aka Shangazi (@fatma_karume) December 4, 2019