Gavana Sonko Aachiwa Kwa Dhamana Huku Akipewa Masharti Magumu


Mahakama Jijini Nairobi imemuachia kwa dhamana Gavana wa Nairobi, Mike Sonko aliyekamatwa siku 5 zilizopita huku akipewa masharti ya kutokwenda ofisini

Sonko ameachiwa kwa dhamana ambapo anaweza kulipa Ksh. Milioni 15 pesa taslimu au kuweka bondi vitu vyake vyenye thamani ya Ksh. Milioni 30

Gavana huyo anayeshtakiwa kwa makosa zaidi 30 yakiwemo ya Utakatishaji Fedha na Rushwa aliomba kuachiwa akieleza nafasi yake kwenye Jamii na kueleza kuwa anahitaji matibabu

Aidha, Sonko ametakiwa kutotumia ofisi yake na akitaka vitu vyake atasindikizwa na Maafisa wa Upelelezi lakini pia hatakiwi kusema lolote kuhusu kesi hiyo kwenye Mitandao ya Kijamii

Mahakama pia, imemtaka kukusanya Nyaraka zake za Kusafiria na kumtaka kuzuia mashabiki wake kutozua vurugu wakati kesi yake inaposikilizwa  -   

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad