Usiku wa jana wa Disemba 12, wakenya wengi hawakuamini macho yao pale walipoweza kuona bendera ya taifa lao iki angaza kwa dakika tatu kwenye ghorofa refu zaidi duniani lililopo Dubai, Burj Khalifa katika maadhimisho ya Jamhuri Day.
Jumla ya rangi nne za bendera ya Kenya ziliweza kushuhudiwa kwenye ghorofa hilo ambazo ni Nyekundu, Nyeupe, Nyeusi na Kijani.
Kenya imekuwa ikisherehekea sikuku ya Uhuru wa taifa hilo kila ifikapo Disemba 12, ambapo kwa hapo jana ikihadhimisha miaka 56.
Inadaiwa gharama ya kurusha tangazo kwa dakika tatu (3), Burj Khalifa inafika Shilingi milioni 156 za Kitanzania.
Hata hivyo haijawekwa wazi kama Kenya ililipia tukio hilo. Inadaiwa ndani ya dakika tatu (3) itakugharimu kiasi cha Shilingi milioni 156 za Kitanzania ili tangazo lako kuonekana kwenye ghorofa hilo refu zaidi duniani kuanzia muda wa saa 2:00 usiku hadi 4:00 wakati wa wikiendi.
Na katikati ya wiki inafikia milioni 292, kama tangazo lako litaonekana ndani ya dakika tatu pekee. Hivyo ukitaka tangazo lako kuonekana lazima uhakikishe umejipanga.
VIDEO: