MREMBO kutoka Bongo Flevani, Gift Stanford ‘Gigy Money’ amefunguka kuwa, alifikia hatua ya kuzaa baada ya mimba zake kibao kuchoropoka katika vipindi tofauti.
Akizungumza na Mikito Nusunusu, Gigy amesema kipindi hajajaaliwa mtoto, alishawahi kupata ujauzito mara nyingi, lakini mimba zilikuwa zikitoka kutokana na vipigo alivyokuwa anavipata kutoka kwa baadhi ya wanaume aliokuwa nao.
“Kizazi changu ni chepesi sana kushika ujauzito, hivyo mara nyingi nilikuwa napata mimba, lakini zinatoka kutokana na vipigo kutoka kwa wapenzi wangu. Kwa hiyo nilipopata mimba ya Mo J, yeye hakunifanyia ukatili ndiyo nikazaa,” alisema Gigy.
Makala: IMELDA MTEMA