Naibu Spika Dkt. Tulia Ackson Afanya Ziara Mkoani Mbeya



Hapo jana Naibu Spika Dkt. Tulia Ackson alifanya ziara katika maeneo mbalimbali ya mkoa wa Mbeya ambapo pia amezidua jumla ya mashina matatu ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) ikiwemo shina la wakereketwa Hasanga, Shina la Makasini stendi pamoja na Stendi mpya.

Pamoja na hayo Dkt. Tulia kupitia taasisi yake ya Tulia Trust ametoa msaada wa jezi za mpira kwa wanavikundi, bima za afya kwa wazee wasiojiweza ambao ni wanachama wa mashina hayo.

Zaidi ya hapo Dkt. Tulia amewataka wananchi kupuuza kauli za baadhi ya viongozi wakiwemo wa vyama vya upinzani wanaowataka kutowatambua na kushirikiana na wenyeviti wa Serikali za mitaa kwa kile wanachodai uchaguzi haukuwa huru na haki.

“Niwaombe sana ndugu zangu tuendelee na ushirikiano wa kujenga taifa letu, usikatae kushirikiana na kiongozi ambaye upo naye. Waswahili tunasema fimbo ya mbali haiui nyoka, sasa wewe unamsikiliza mtu yupo Dar es salaam anatoa tamko na wakati huohuo yeye mwenyewe anashirikiana na viongozi wakuu alafu anakudanganya wewe usishirikikiane na viongozi wako," amesema.

Ameendelea kwa kusema, "Tushirikiane na viongozi tuliowachagua, na tunasema tumewachagua kwasababu ukiwa uwanjani ukipigwa kwa penati au dakika tisini hata kama ni dakika za nyongeza kote ni kupigwa tu na wakubali yakuwa wamepigwa,”.


Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad