HATIMAYE Cyrill Kamikaze Afunguka TUHUMA za Kuingilia Penzi La Vanessa Mdee na JUX

Msanii maarufu wa mitindo ya Rap hapa Bongo, Cyrill maarufu kwa jina, Kamikaze amefunguka kuwa licha ya mwanadada Vanessa, ambaye alikuwa shemeji yake kumzungumzia vibaya kipindi cha nyuma wakati yuko kwenye migogoro ya kimapenzi na Jux yeye hawezi kumuhukumu kwa chochote.

Akizungumza na moja ya media kubwa hapa bongo Kamikaze amesema "Hilo lishapita labda tuweke msumari wa mwisho, sikuwahi kufanya chochote wala kuongea lolote kitu kilichotokea ni kati yake na Jux kwenye mapenzi yao, mimi sijawahi kuingilia na kujua chochote kama aliongea hivyo ni fresh"

Aidha Kamikaze ameongeza kwa kusema kuwa "Kwa yeye kuongea vile sijui alikuwa katika hali gani na alimaanisha nini, sijawahi kukaa naye kumuuliza lakini nina imani hakuongea kile kitu kwa kukimaanisha, unajua kuna muda unaweza ukaongea kitu kwa kuwa una hasira au mawazo kwa sababu ya vitu vingi, sijawahi kumhukumu na siwezi kurudisha neno lolote.
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad