'Hayawahusu, Mimi na Uchebe Tunawachora' - Shilole



Msanii Shilole, amezungumzia kitendo cha yeye kuonekana amenuna katika zoezi la kulishana keki na mume wake, wakati wa kusherehekea kumbukumbu ya siku yake ya kuzaliwa na kusema kuwa watu waache kufuatilia maisha yake na kwamba yeye na mume wake wako sawa.

Akizungumza leo Disemba 23, 2019 na EATV &EA Radio Digital, baada ya kuulizwa sababu iliyopelekea akanuna ilihali ile siku ilikuwa ni muhimu kwake, Shilole amesema kuwa ule ulikuwa ni ununaji wa kike tu.

"Ni vitu vya kawaida tu na ule ni ununaji wa kike, kuna vitu vidogo vilitokea vika dissapoint sura yangu, mimi sio muongo na kitu kikitokea na react vibaya, tusipangiane maisha kila mtu ana mambo yake, sisi hatuna shida tuna waangalia tu, watuache mimi na mume wangu tunajuana wenyewe" amesema Shilole.

Juzi Disemba 20, wakati wa kumbukizi ya siku ya kuzaliwa kwake, Shilole alionekana kununa wakati akimlisha keki mume wake huyo, ambapo baada ya video hiyo kusambaa mitandaoni, mashabiki zake walimuandama na kumsema kuwa tabia aliyoinesha hadharani haikuwa nzuri.
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad