ILIKUWA siku ya Sikuku ya Noeli almaarufu Christmas mnamo mwaka 1971. Mkuu mpya wa Mkoa wa Iringa aliyehamishiwa hapo akitokea Mtwara, Dkt. Wilbert Kleruu, msomi wa Shahada ya Uzamivu (PhD) wa Uchumi wa kijamaa katika Kilimo aliuawa na Mkulima aitwaye Said Mwamwindi
Kipindi hicho kulikuwa na kampeni ya kutaifisha mashamba ya wakulima wakubwa na kuyafanya mashamba ya kijiji. Na Dkt. Kleruu alipelekwa Iringa ili akatekeleze kazi hiyo kwani kipindi hicho Iringa ilikuwa na wafanyabiashara wakubwa waliomiliki mashamba makubwa ya Kilimo hasa maeneo ya Isimani
Katika eneo hilo la Isimani kulikuwa na mkulima mmoja aliyekuwa anamiliki takribani hekari 400 za mashamba na mfanyabiashara aliyekuwa anamiliki majumba Iringa mjini - Said Mwamwindi
Kwa wakati ule ilishauriwa angalau kila mtu awe na shamba lisilo zidi hekari 4. Jambo ambalo lilileta mvutano mkubwa kati ya wakulima wakubwa na Serikali
Sasa siku hiyo ya Christmas, Dkt. Kleruu alikwenda Isimani akiwa katika utekelezaji wa sera ya kutaifisha mashamba. Moja kwa moja alikwenda hadi shambani kwa Mwamwindi, na kumkuta analima
Mkuu huyo wa Mkoa akamuuliza mbona unalima shamba lako mwenyewe na si la kijiji? Mwamwindi akajibu, sioni tatizo hakuna mtu shambani, leo ni Jumapli tena ni sikukuu
Maneno yale yalimuudhi Dkt. Kleruu, ambaye alikuwa akisifika kwa ukali, kutekeleza sera za serikali na maneno makali au kutukana watu hadharani pale wanapo fanya makosa
Dkt. Kleruu baada ya kuudhika alimtukana Mwamwindi tusi lililomlenga mama yake ambaye tayari alikuwa marehemu. Mwamwindi alihoji inakuwaje anamtukania mama yake, huku akimuonyesha kaburi alimozikwa?
Mkuu wa Mkoa, aliendelea kuja juu, huku akisema kaburi ndio nini? Huku akilipiga mateke kaburi la Mama yake Mwamwindi. Kwa kabila la wahehe makaburi yana heshima yake, kwani ndipo nyakati nyingine hutumika katika sala, matambiko na mila kadha
Kitendo kile kilimghadhabisha Mwamwind, na kuanza kukimbia kuelekea nyumbani. Mkuu wa Mkoa akadhani Mwamwindi anamkimbia, akaamua kumfuata
Alipofika nyumbani, tayari Mwamwindi alisha ingia ndani na kuchukua bunduki yake, Dkt. Kleruu baada ya kuona hali ile ma
Mbona hujatumalizia story hii. Naomba utumalizie maana wengine tumewahi sikia nyimbo za mbaraka mwishehe mwaluka ikimuimba dkt kleruu ila hatukujua kisa kilichomletea kuuawa.
ReplyDeletetulizuia wakulima wawekezaji wa ndani na leo tunatafuta wawekezaji toka nje !! hua tunakosea lakini hatukiri makosa na kwa kua hatukiri tutazidi kukosea
ReplyDelete