Ifahamu Historia ya Mwigizaji Brad Pitt




Desemba 18, 1963 alizaliwa mwigizaji na prodyuza wa filamu nchini Marekani maarufu kwa jina la Brad Pitt.

Jina lake halisi ni William Bradley Pitt. Nyota huyo ametunukiwa tuzo nyingi na ameshiriki pia katika utoaji wa tuzo mbalimbali hapa ulimwenguni.

Miongoni mwa tuzo ambazo Brad Pitt ametunukiwa ni ile ya Academy na Primetime akiwa na kampuni lake la Plan B Entertainment.

Brad Pitt alizaliwa mhini Shawnee huko Oklahoma kwa wazazi William Alvin Pitt ambaye alikuwa mfanyakazi wa kampuni ya malori na mama yake alifahamika kwa jina la Jane Etta aliyekuwa mshauri wa shule.

Licha ya kuzaliwa huko Oklahoma lakini alikulia huko Springfield, Missouri ambako wadogo zake wengine Douglas Mitchell (1966) na Julie Neal (1969).

Alikulia katika familia ya Kikristo ya waumini wa kanisa la Baptist.

Baadaye Brad Pitt aligeuka na kuachana na imani hiyo na kujiunga na imani za miungu. Akiwa Springfield alipaita mahali pale kuwa ni nchi ya Mark Twain na Jesse James kutokana na kuwa ni eneo la milima milima na maziwa.

Alisoma katika shule ya sekondari ya Kickapoo ambako alikuwa miongoni mwa vijana waliokuwa wakicheza gofu, kuogelea na tenisi. Alishiriki katika midahalo mbalimbali shule hapo.

Baada ya kuhitimu masomo hayo aliingia katika Chuo Kikuu cha Missouri mnamo mwaka 1982 ambako alisoma uandishi wa habari na matangazo. Alikuwa akipenda sana filami katika maisha yake.

Akiwa chuo kikuu aliwahi kuwataja mashujaa wake katika filamu waliokuwa wakimvutia Gary Oldman, Sean Penn ana Mickey Rourke.

Kwa mara ya kwanza kabisa ulimwengu ulimfahamu Brad Pitt alipoonekana katika filamu ya Thelma & Louise (1991) baadaye akaanza kuonekana katika filamu nyingine kama A River Runs Through It (1992), Legends of the Fall (1994) na Interview with the Vampire (1994).

Brad Pitt hakuishia hapo alionekana katika filamu Fight Club (1999), Ocean's Eleven (2001), Ocean's Twelve (2004) na Ocean's Thirteen (2007). Brad Pitt alipata mafanikio zaidi sokoni katika filamu Troy (2004), Mr. & Mrs. Smith (2005), World War Z (2013), na  Once Upon a Time in Hollywood (2019).

Hata hivyo amekuwa maarufu katika filamu ya Inglourious Basterds aliyofanya mwaka 2009 chini ya director mahiri na maarufu katika kuongoza filamu za kivita Quentin Tarantino.



Mnamo mwaka 2014 alimwoa mwigizaji wa kike wa Marekani Angelina Jolie na kufanikiwa kuzaa naye watoto watatu na wengine watatu waliweza kuwaasili.

Mnamo mwaka 2016 Jolie alitaka talaka kutoka kwa Brad Pitt na talaka ilitolewa rasmi mwaka 2019.

Kabla ya kuwa na Angelina Jolie aliwahi kuwa katika mahusiano na mwigizaji mwingine Jennifer Aniston aliyemwoa mnamo mwaka 2000 na waliachana miaka mitano baadaye.

Kwa miaka mingi sasa Brad Pitt amekuwa akichukuliwa kuwa ni miongoni mwa watu wenye mvuto duniani.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad