JE Wajua Kwanini Mbu Hasambazi Virusi vya Ukimwi VVU?


Kila inapofika Desemba mosi ya kila mwaka ni siku ya kimataifa ya Ukimwi Duniani.

Siku hii iliadhimishwa wiki mbili zilizopita kwa wadau kutoa elimu ya mambo mbalimbali kuhusu ugonjwa huu.

Mmoja wa wasomaji aliuliza swali kama mbu anaweza kusambaza virusi vya Ukimwi (VVU)kama anavyofanya kwa vijidudu wa malaria kutoka mtu mmoja kwenda mwingine. Ni kweli mbu ndiye anayebeba aina nyingine za virusi ikiwamo virusi vya homa ya Manjano, Dengue na Chikungunya.

Zipo takribani jamii 3,500 za wadudu hawa (mbu) wanaoneza magonjwa mbalimbali lakini hakuna hata mmoja anayeweza kusambaza VVU. Leo nitawajuza sababu kuu tatu za kisayansi zinazotoa ufahamu kwanini mbu hawezi kueneza VVU.

Sababu ya kwanza ni mfumo wa unyonyaji damu wa mbu

Mfumo huu unakinyima nafasi kirusi cha Ukimwi kuenezwa kutoka kwa mtu mmoja kwenda kwa mwingine, hii inatokana na maumbile na kazi ya mfumo wa uumaji na unyonyaji damu kwa kutumia mirija yake.


Mdomo wa mbu una sehemu sita, kati ya hizo sehemu nne hukita katika ngozi ya mwanadamu au mnyama anayemuuma. Sehemu nyingine mbili zina mirija miwili, mmoja wa mrija huo huwa na kazi ya kutiririsha mate kwenda kwa mtu anayemuuma na mrija mwingine ni kufyonza damu ya mwanadamu kuja kwa mbu. Mfumo huu wa mirija miwili ndiyo sababu ya mbu kushindwa kueneza VVU kwa kuwa hata akifyonza damu yenye VVU atakapokwenda kwa mtu wa pili atamwingizia mate na si damu yenye VVU aliyofyonza awali. Hivyo mbu akikuuma ni lazima acheue mate yaingie kwa mtu na kisha kufyonza damu na wala si kufyonza damu na kuitema kwa mtu mwingine.

Sababu ya pili ni kumeng’enywa kwa kirusi katika tumbo la mbu. Tofauti na vijidudu vingine, VVU haviwezi kuzaliana na kuongezeka katika utumbo wa mbu na vikiingia humo huvunjwa vunjwa. Katika mwili wa mwanadamu kirusi cha Ukimwi hujipachika katika chembe hai nyeupe zijulikanazo kitabibu kama T-Cells na kuanza kutumia malighafi za seli hizo ili kuanza kuzaliana. Ndani ya tumbo la mbu hakuna chembe hai hizi, hivyo kumnyima nafasi ya kirusi kuzaliana katika tezi zinazohifadhi mate ya mbu. Kama kirusi cha Ukimwi kitaingia tumboni mwa mbu humeng’enywa na damu iliyofyonzwa katika mfumo wa usagaji wa chakula wa mbu. Wakati wa umeng’enywaji damu virusi hivyo huharibiwa.

Mwananchi
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad