Jeshi la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam limesema linamshikilia ofisa programu wa kituo cha sheria na haki za Binadamu (LHRC), Tito Magoti kwa mahojiano .
"Tunamshikilia Tito Magoti (26), Mkazi wa Ubungo Kibo, Afisa Programu wa Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu ( LHRC ) pamoja na Watu wengine watatu kwa uchunguzi na mahojiano kwa tuhuma za makosa ya jinai ”- Amesema Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar Es Salaam, Lazaro Mambosasa.
Amesema Magoti na wenzake amekamatwa na Polisi leo Ijumaa asubuhi maeneo ya Mwenge na wote kwa pamoja wanaendelea kuhojiwa kwa tuhuma za makosa ya jinai.
“Tito Magoti hakutekwa bali amekamatwa na Polisi leo saa tano asubuhi maeneo ya Mwenge na yupo katika mikono salama, yeye na wenzake watatu wanaendelea kuhojiwa na watafikishwa Mahakamani baada ya kukamilisha uchunguzi na mahojiano”amesema Mambosasa