Jeshi la Polisi Mkoa wa Mwanza Latoa Ufafanuzi Kukamatwa kwa Dereva wa Katibu Mkuu CHADEMA Na Afisa Habari


Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mwanza ACP.Muliro Jumanne amekanusha taarifa zilizokuwa zinasambaa katika mitandao ya kijamii zikieleza kuwa kuna wanachama wa chadema wametekwa jijini hapa.

Muliro amesema hakuna utekaji uliotokea bali wanachama hao walikamatwa na jeshi la polisi kwa ajili ya mahojiano baada ya kupata taarifa kutoka kwa raia wema.

Akizungumza na Waandishi wa Habari,  ACP Muliro Muliro amesema siku ya Desemba 29, Mwaka huu Majira ya 15:00 Mtaa wa Mahina Kata ya Mahina wilayani Nyamagana kulipatikana taarifa toka kwa raia wema kuwa kumeonekana watu wawili waliohisiwa kuwa siyo watu wema wakiwa karibu na Hoteli ya Paradise na kuingia nyumba jirani iliyokuwa karibu na hoteli hiyo.

Kamanda Muliro, amesema baada ya kupatikana taarifa hizo jeshi la polisi  lilifanya ufuatiliaji wa haraka na kufika eneo hilo na kuwakamata watu hao wawili, ambao katika mahojiano ya awali walikataa kutoa utambulisho wao kuwa wamefika maeneo hayo kufanya shughuli gani.

"Walichukuliwa na kupelekwa kituo cha polisi kati na kutoa ushirikiano kwa askari pia kutaja majina yao kuwa ni Abdukarimu Muro (31), mchaga Afisa Habari Katibu Mkuu CHADEMA Mkazi wa Kinondoni B, Dar es Salaam na Said Haidani (30), Dereva wa Katibu Mkuu CHADEMA, Mkazi wa Mbezi Kimara Dar es Salaam wameambatana na Katibu Mkuu CHADEMA, Mh. John Mnyika na polisi waliwaachia baada ya kujiridhisha hawakuwa wahalifu waliachiwa huru," amesema ACP Muliro.

Aidha Jeshi la Polisi Mkoa wa Mwanza limetoa onyo kwa kwa watu wasiokuwa na taarifa rasmi na wenye tabia za kuzusha mambo hasa ya watu wanapokamatwa wao husema kuwa wametekwa na hivyo kuzusha taharuki kwa jamii kwani matendo hayo ni makosa na hatua za kisheria zitachukuliwa dhidi yao watakapobainika.
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad