JOKATE "Ukibaka Mtoto KISARAWE Tunakukomesha"

Mkuu wa Wilaya ya Kisarawe Jokate Mwegelo @jokatemwegelo amesema vitendo vya ubakaji havikubaliki Wilayani humo na wanafanya juhudi za kuwalinda Watoto dhidi ya vitendo vya ukatili ambapo Kwa Mwaka huu tu Watu wanane wamehukumiwa miaka 30 Jela kwa ubakaji, akiwemo Baba aliyembaka Binti yake wa Kumzaa na tayari Baba huyo amehukumiwa na Mahakama ya Wilaya Kisarawe kwenda jela miaka 30.

“Tumesimamia haki ya huyo Binti aliyebakwa na Baba yake mzazi, Binti anasoma darasa la nne, pia kuna Babu kamlawiti Mjukuu wake, Ijumaa iliyopita Kituo Cha Polisi Kisarawe limefunguliwa shauri baada ya ustawi wa jamii kuripoti Binti kabakwa na kupewa mimba na Mchungaji wa kanisa liko nje ya Kisarawe”- DC JOKATE

”Hivyo kwa Mwaka huu kupitia Mahakama yetu ya Wilaya Kisarawe tumehukumu Watu wanane waliobaka, Miaka 30 kila mmoja na Watu wawili waliowapa Mabinti mimba miaka 30 kila mmoja, nipongeze Mahakama, kitengo chetu cha ustawi wa jamii, Polisi na Afisa Eimu Msingi/Sekondari”-DC JOKATE

“December 10,2019 kupitia Dawati la Jinsia na Watoto Kisarawe kwa uratibu wa OCD Eva tumezindua Mpango Mkakati wa Kudhibiti Ukatili Wa Kijinsia Wilaya ya Kisarawe 2020 unaojumuisha kutoa Elimu, kushirikisha Jamii kusimamia hili na kuhamasisha utoaji taarifa kwa wakati”-DC JOKATE
Tags

Post a Comment

2 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Ubakaji unashamiri kutokana na tabia za wanawake kupenda wanaume wenye hela, wenye magari na kazi nzuri hivyo kufanya wale wanaume wasio na kitu kukosa watu wa kuwaliwaza ijapokuwa kuna wengine ni wababa wenye familia zao lakini kutokana na ushetani walionao wanadiriki kubaka watoto hivyo sababu zinazochangia ubakaji zipo nyingi sana.

    ReplyDelete
  2. Hao waliohukumiwa miaka 30 wanatakiwa wachapwe viboko 30 kila mmoja yaani kila mwezi anachapwa viboko saba.

    ReplyDelete

Top Post Ad

Below Post Ad