JPM "Wahudumu wa ATCL Wapuuzeni Wanaosema Ninyi Wabaya, Ninyi ni Wazuri"

Rais Magufuli wakati akipokea ndege iliyokuwa imezuiliwa Canada amebainisha kuwa ndege mpya tatu zilizobaki zitawasili mwakani ambapo moja (Bombardier Q400) itawawasili Mwezi Juni na nyingine mbili ni Air-Bus 220-300 ambapo moja itawasili mwezi Juni na nyingine mwezi Julai 2021

Lakini pia, ameweka wazi mpango wa Serikali kutaka kununua ndege ya mizigo itakayosafirisha shehena ya bidhaa za maua na mbogamboga kwa lengo la kuongeza fursa za uwekezaji na biashara kwa wakulima nchinini

Katika kupongeza jitihada zilizofanyika hadi ndege hiyo ikawasili Jijini Mwanza, Rais Magufuli ameagiza Marubani watatu wa Kitanzania walioiongoza ndege hiyo wapewe Tsh. Milioni mbili kila mmoja kama pongezi kutoka kwake

Aidha, katika hatua nyingine akizungumzia Wahudumu wa ATCL amesema, “Wahudumu wa ATCL wapuuzeni wanaosema ninyi wabaya, ninyi ni wazuri, na ‘shape’ zenu ni nzuri, roho zenu ni nzuri na sauti zenu ni nzuri. Chapeni kazi.”
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad