Jux Atamani Mtoto wa KIKE, Aeleza Mipango yake


Mkali wa muziki wa Rnb Juma Jux amefunguka kuwa anatamani kupata mtoto wa kike kwa sababu anataka amlee kwenye mazingira ya kujitegema zaidi.


Akipiga stori kupitia EATV & EA Radio Digital, Jux amesema sababu za kutaka mtoto wa kike ni anaamini kwenye kuwekeza kwa mwanamke kwasababu atakuwa na uwezo wa kusaidia watu wengine.

"Nimesema mtoto wangu wa kike wa kwanza, ila anaweza akawa hata wa pili kama nikipata wa kiume wa kwanza ila awe mtoto wa kike, nitamlea katika akili ili aweze kujitegemea zaidi, naamini  kwenye kuwekeza kwa mwanamke ili ajitegemee kwa sababu kuna vitu vingi sana vitakuwa vizuri na ataweza kusaidia watu wengi sana" amesema Juma Jux.

"Mwanamke ambaye anaweza kujitegemea atakuwa vizuri kwenye maisha kuliko anayemtegemea mtu, kwahiyo mimi hicho ndiyo kitu ambacho nakiangaliaga sana, hata kwa mtu ambaye nakuwaga naye kwenye mahusiano namuangaliaga kama ana uwezo wa kujitegemea, na hata kama hawezi nitamtengenezea mazingira aweze kujitegemea bila mimi" ameongeza.
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad