Kala Jeremiah Afunguka Kuhusu BARUA Aliyoandikiwa na Basata...


Rapper Kala Jeremiah amesema kuwa kitendo cha Serikali kumuandikia barua ya pongezi na shukrani kimemuongezea chachu na kuongeza ubunifu zaidi katika kazi yake ya sanaa.
Baraza la Sanaa la Taifa (BASATA) ambaye ndio msimamizi wa shughuli za sanaa hapa Nchini walimuandikia msanii huyo barua tarehe 05/12/2019 ya shukrani na pongezi baada ya kuguswa na mchango wake kupitia sanaa.

Kala amesema barua hiyo anaichukulia kama ni Tuzo kwani kwa miaka kadhaa kumekosekana Tuzo licha ya Wasanii wengi kufanya vizuri.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad