Rais wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) Wallace Karia amechaguliwa kuwa Rais mpya wa Baraza la Vyama na Vilabu Afrika Mashariki na Kati (CECAFA) kwenye uchaguzi uliofanyika leo majira ya saa 9 alaasir kwenye Hotel ya Silver Springs Hotel, Lugogo Kampala nchini Uganda.
Karia amechaguliwa kwenye nafasi hiyo, baada ya kupitishwa bila kupingwa kuwa Rais wa Baraza la Vyama na Vilabu Afrika Mashariki na Kati (CECAFA).
Katika uchaguzi huo, Karia alikuwa ni mgombea pekee na wajumbe waliamua kutopiga kura na badala yake kumpitisha awe Rais wa baraza hilo.
Kwa matokeo hayo sasa Rais Karia atatumikia nafasi hiyo kwa muda wa kipindi cha miaka 4, huku makamu wake akiwa,Francis Amin wa Sudan Kusini aliibuka mshindi akimpiku Isayas Jira Bosho wa Ethiopia na wajumbe ni Esayas Abraham na Sekemana.