Kenya: Mabasi Yagongana, Watu Saba Wafariki Dunia



Mabasi Modern Coast hayo yamegongana katika eneo la Kiongwani karibu na Kijiji cha Salama katika Barabara Kuu ya Mombasa-Nairobi, Kenya ambapo watu watano walifariki papo hapo

Watu 62 walijeruhiwa na kati yao wawili walifariki na kuongeza idadi ya vifo hadi saba katika ajali hiyo ambapo gari moja lilikuwa linatokea Malaba na lingine likitokea Mombasa

Kamanda wa Polisi wa Makueni, Joseph Napeiyan amesema ajali hiyo imetokea Saa Nane Usiku wa kuamkia leo baada ya gari lililokuwa likitokea Mombasa kuhama nafasi yake

Kwa mujibu wa taarifa kutoka Kenya, ajali hiyo imetokea siku moja baada ya ajali kama hiyo kutokea katika eneo hilo kati ya basi la Modern Coast na Tahmeed.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad