KENYA: Mwili wa mtu mmoja na gari lake lililozama baharini waopolewa Mombasa


Mwili wa mtu ambaye gari lake liliingia baharini katika kivuko cha likoni mjini Mombasa mapema siku ya Jumamosi umeopolewa. Shirika la hudumu za Ferry nchini Kenya KFS limesema kwamba gari la John Mutinda lilishuka katika mreremko kwa kasi ya juu. Kisa hicho kinarejesha upya kumbukumbu za mkasa mwengine mwezi Septemba mwaka huu ambapo Mariam Kighenda na mwanawe Amanda Mutheu walikufa maji.

Iliwachuku waokoaji takriban siku 13 kuopoa miili pamoja na gari walilozama nalo.

Taarifa ya KFS kuhusu kifo cha Mutinda ilisema: Dereva alikuwa akiendesha gari aina ya saloon ambaye nambari zake za usajili hazijafichuliwa baada ya kununua tiketi aliteremka kwa kasi katika mteremko wa feri na kuingia baharini.


Breaking News
@News_Kenya
Body of man whose car plunged into Indian Ocean retrieved: The Kenya Ferry Services said John Mutinda's car sped off the ramp at high speed. 

Shirika hilo liliongezea kwamba dereva huyo alikataa kusimamisha gari hilo licha ya juhudi kadhaa za maafisa wa feri kumsimamisha.

Maboti ya uokoaji ya KFS , wanamaji wa Kenya Navy na maafisa wa polisi wakishirikiana na waokoaji wengine yalifika katika kivuko hicho mara moja na kuanzisjha operesheni ya kulisaka gari hilo mara moja.

Gavana wa Mombasa Hassan Joho mapema alikuwa amesema kwamba serikali ya kaunti hiyo ilikuwa imepeleka kitengo chake kushirikiana na wakojia wengine wa idara tofauti za serikali
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad