Kinacho Waweka Njia Panda Wadada Katika Umri wa Kuolewa na Kujikuta Umri Umeenda

Zama hizi hitajio la ndoa limekuwa ni kubwa zaidi, lakini jambo la kusikitisha ni kuwa ndoa zimekuwa ngumu sana. Na mabinti wamebaki njia panda (Dillema). Miongoni mwa mambo yanayowafanya wawe njia panda ni hali.

#Wanataka wenye mali,
wenye mali wengi hawana dini wala ucha mungu. Na wenye ucha mungu wanatakiwa na wengi. Jambo ambalo limefanya wawe wanachagua zaidi. Njia panda.

#Wanataka Mahandsome,
Mahandsome wengi ni Mario wanatumia uhandsome wao, kuwatumia mabinti tu . Na mwisho kuangukia Kwa wanawake wenye pesa zao. Na wao kuwa mamario. Na wenye dini ni kinyang'anyiro kwa mabinti. Njia panda.

#Wanataka wanaume wa pekee yao, wapeke yao ni maskini.
Na mabinti hao hawako tayari kwenda kuishi maisha ya kimaskini kupambana pamoja na mume ili wafanikiwe pamoja. Njia panda.

#Wanataka wenye elimu za vyuo vikuu kama wao, wenye elimu hizo hawawataki kwasababu ya changamoto wanazoziona vyuoni, wanataka wenye elimu ndogo zaidi. Njia panda.

#Wanataka waliojiimarisha kiuchumi hata kama ni uchumi wa wastani na awe na dini.
Hao wana namna hiyo wapo lakini Kwa kumuogopa Allah wameoa mapema na wana wake zao. Kwa hivyo ndoa hapo hi matala, mabinti hawako tayari na ndoa za wake wengi. Njia panda.

#Wanataka vijana wenye Elimu, vijana hao wapo lakini ndio kwanza wanaanza maisha, wana chumba cha kupanga. Wao wanataka wenye uchumi mzuri. Wenye uchumi mkubwa umri umekwenda. Njia panda.

#Wanataka waume wenye misimamo yao ya kimadhehebu, wanaume wa namna hiyo imma ni wachache au sio chaguo lao. Njia panda.

#Kuhadaiwa na mapenzi yasio rasmi, miaka kadhaa, wanakuja waposaji hawakubali. Mara wanatelekezwa. Njia panda.

#Wanaifanya ndoa ni second selection, maisha kwanza ndoa baada, wanapofeli katika malengo ya kimaisha ndoa wanaitafuta ndoa. Muda umeenda mvuto umepotea, kaingia kasoro tayari kwanini achelewe. Njia panda.

#kuhadaiwa na uzuri wao, na kukataa ndoa. kwa madai wao ni warembo kwa hivyo wataolewa tu. Na wakasahau wa simu sio housing bali ni software. Matokea umri unakwenda na wanabaki kuwa ni sehemu ya starehe tu kwa wanaume na sio wake wakuwekwa ndani. Njia panda.

Mara paaa miaka 30 hiyo, mwisho wa siku anaekuja na aje. Na kuanza wana nuksi, hali ya kuwa nuksi wamejitia wenyewe. Na matokeo yake mbio kwa waganga matapeli haziishi. Dillema/njia panda hiyo imwaacha mabinti wengi wanaugulia maumivu ya kutendwa katika magenta. Na mwisho ni maamuzi ya kutafuta japo mtoto wa nje wasijekufa bila ya kuacha kizazi.

Wasichokijua mabinti wengi ni kuwa sifa za mume kuoa ni mbili tu hakuna ya tatu. Na asipoozeshwa mwenye sifa hizo basi lazima kuwe na maharibiko
HII NI FAIDA MABINTI WOTE
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad