Latra Yawakomalia Wanaopandisha Nauli Mabasi ya Mikoani


Dar es salaam. Mamlaka ya Udhibiti wa Usafiri Ardhini (Latra) imesema inapambana na wanaopandisha nauli za mabasi kutoka Dar es Salaam kwenda mikoa mbalimbali nchini katika kipindi cha  kuelekea sikukuu za mwisho wa mwaka.

Akizungumza na Mwananchi leo Jumamosi Desemba 21, 2019  ofisa leseni wa mamlaka hiyo, Leo Ngowi amesema wameanza kufanya ukaguzi, ikiwa ni pamoja na kuwakamata mawakala wanaotoza nauli kubwa.

"Tumeanza kufanya ukaguzi tangu jana na kubaini mabasi yanayotoka Dar es Salaam kwenda Mwanza na Kahama nauli zimeanza kupanda kiholela. Tumeshachukua hatua na wapo waliotozwa faini,” amesema Ngowi.

Kuhusu uhaba wa mabasi amesema umetokana na abiria kuongezeka, hasa wa mikoa ya Kaskazini.

“Mikoa yenye idadi kubwa ya abiria ni Tanga, Kilimanjaro, Arusha, Morogoro na Dodoma. Katika kuhakikisha hali inakuwa shwari tumeongeza mabasi kwa kutoa leseni za magari madogo yenye uwezo wa kupakia abiria 40,” amesema.
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad