Ligi ya Italia Serie A kutumia Picha za Nyani Kupinga Ubaguzi , Wadau Walaumu “Je Hakuna Watu Wenye Busara Wanaoendesha Ligi ya Serie A?”


Ligi kuu ya Italia Serie (A) ilipozindua kampeni yake ya hivi karibuni inayopinga ubaguzi wa rangi, matokeo hayakuwa ya kuridhisha. Kundi la kufuatilia ubaguzi wa rangi nchini Italia, limesema kwamba ”huu ni utani mbaya”, Aliyekuwa mshambuliaji wa Norway Jan-Aage Fjortoft ameuliza: ”Watu wana matatizo gani??? Je hakuna watu wenye busara wanaoendesha ligi ya Serie A?”



Sababu za ukosoaji? Kampeni iliyoanzishwa na msanii Simone Fugazzotto, ilikuwa na michoro ya nyani watatu, waliopakwa rangi za timu tofauti kwenye nyuso zao.

Fugazzotto anasema kwamba madhumuni yake yalikuwa ni kuonesha watu wabaguzi kwamba ”watu wote ni nyani”.

Lakini katika muktadha wa soka, hususan nchini Italia, ni rahisi kuona kwa nini watu wengi wanaichukulia kama kampeni inayopotosha zaidi.

Kelele za kibaguzi
Chris Smalling na Romelu LukakuHaki miliki ya Smalling akikutana tena na Lukaku na kuzua mjadala kuhusu ubaguzi wa rangi katika soka ya Italia
Ili uweze kuelewa ghadhabu ya watu, ni vizuri ukarejea katika masuala ya msingi.

Nyimbo za kibaguzi limekuwa tatizo kubwa katika soka ya Ulaya tangu wale wachezaji weusi walipoanza kujumuishwa katika mechi tangu miaka ya 1970. Lakini licha ya kwamba hilo limekuwa likijitokeza katika ligi mbalimbali – ikiwemo Ligi ya Premia, ligi inayoangaziwa zaidi duniani – Italia imekuwa na wakati mgumu sana katika hili.

Kundi fulani kuzomea mchezaji ndio kubaya zaidi kuliko makelele ya mtu mmoja jambo ambalo Italia imeshindwa kabisa kulidhibiti.

Baadhi ya mashabiki wanaamini kwamba ubaguzi wa rangi dhidi ya wachezaji weusi hauna tofauti na maovu mengine kwa wachezaji wa timu pinzani mfano kudhihaki namna walivyonyolewa ama uzito wao.

Wengine wanadai kwamba nyimbo za kibaguzi ni mfano wa mbinu nyingine za kutafuta ushindi wala siyo ubaguzi.

Hii ni moja ya sababu iliyotolewa na baadhi ya mashabiki wa Inter Milan walipojitetea kuhusu madai ya unyanyasaji yanayolenga mchezaji fulani, Romelu Lukaku, hayo ni kulingana na mashabiki wa timu ya Cagliari yaliyotolewa Septemba.

”Nchini Italia tunatumia baadhi ya njia kusaidia timu zetu na kujaribu kutia timu pinzani mchecheto wala siyo ubaguzi lakini ni mbinu ya kuwachanganya”, wamesema hivyo.

Lakini wachezaji weusi wanapolengwa kwa namna hii, mara nyingi hutumia njia ya kuwafananisha na nyani. Athari yake ni kwamba wachezaji weusi wanafananishwa na nyani; kwamba wao hawana thamani.

Miongoni mwa wale ambao wanahoji kampeni hiyo ni pamoja na aliyekuwa mshambuliaji wa Everton na Man City Sylvain Distin.

“Sielewi vile unavyoweza kupinga ubaguzi wa rangi na kitu ambacho kinafananishwa na ubaguzi wa rangi,” Distin ameiambia BBC.

“Haileti maana kwa kweli kiasi kwamba nilijaribu kusikiliza tena mahojiano mengi kadiri ya uwezo wangu aliyofanya msanii huyo.

“Ni kweli kwamba alitengenza michoro mingi, ujumbe na kujenga taswira inayozunguka nyani kwa kipindi cha miaka mitano hadi sita, na kulingana na kile ambacho msanii huyo anaweza kusema ni kwamba sisi sote ni nyani. Lakini hilo si sawa.”

Kwanini walifanya hivyo?

Mashabiki wa Napoli wakiwa wameshika mabango yenye picha ya Kalidou KoulibalyHaki miliki ya Mashabii wengi wa Napoli walikiwa karibu na Kalidou Koulibaly baada ya kurushiwa maneno ya ubaguzi wa rangi – kisha wakampigia makofi ya kejeli
Kama Distin anavyosema, Fugazzotto amekuwa akitumia nyani katika usanii wake, na hivyo huenda isiwe sawa kumkosoa kwa kutekeleza kazi yake.

Na Fugazzotto amesema kwamba kilichompa motisha katika kazi zake ni kuona jinsi baguzi unavyoendelezwa katika mechi zilizochezwa msimu uliopita ambazo alizitazama.

“Niliamua kutumia mchoro wa nyani kuzungumzia ubaguzi kwasababu ni kama fumbo kwa mwanadamu. Mwaka uliopita nilikuwa katika uwanja mmoja wa michezo kutazama mechi kati ya Inter na Napoli ambapo mshambuliaji Kalidou Koulibaly alibaguliwa vibaya na nikahisi kufedheheshwa, kila mmoja alikuwa akipiga kelele na kumwita Koulibaly, ‘nyani’ mchezaji ambaye namuheshimu sana,” amesema.

“Nimekuwa nikitengeneza michoro ya nyani kwa kipindi cha miaka mitano hadi sita iliyopita, kwa hiyo niliwaza kwamba mchoro huu ungetoa taswira ya kuwa sisi sote ni nyani, nikatengeneza nyani la nchi za magharibi kwa kulipaka rangi ya buluu na macho meupe, nyani wa Asia nikamtengeneza macho ya lozi na nyani mweusi nikamweka katikati kitovu cha kila jambo. Nyani hao walikuwa chanzo cha kufahamisha watu kwamba kila mmoja ni sawa na hakuna tofauti ya mwanadamu na nyani, sote tunafanana. Ukweli ni kwamba, sisi sote ni nyani.”

Lakini jambo linalozua maswali ni vile ligi hiyo ilivyomuagiza Fugazzotto kutengeneza michoro hiyo iwapo walijua kwamba kazi zake zinahusisha michoro ya nyani pekee.

Hata hivyo, maneja wa klabu ya ligi ya Serie A Luigi De Siervo ameonekana kuwa mkaidi.

“Usanii wa kweli ni uchokozi, alijibu hivyo baada ya kutakikana aelezee kuhusu kampeni hiyo.

“Michoro ya Simone inaakisi maadili ya uchezaji wa usawa na uvumilivu kwa hiyo itasalia katika makao yetu makuu”.

“Ligi ya serie A inachukulia msimamo mkali dhidi ya ubaguzi. Tunafahamu kwamba ubaguzi ni tatizo kubwa na tata, kwa hiyo tunakabiliana nalo kwa namna tatu – kitamaduni, kupitia haki za kisanii kama vile za michoro ya Simone, kupitia michezo kama vile katika klabu na wachezaji, na pia kukandamiza suala hilo jambo ambalo limewezekana kwa ushirikiano na polisi.

”Kwa kuzingatia hayo, tunaimani kwamba tutaweza kushinda vita dhidi ya jinamizi hili ambalo linaendelea kusambaa katika mchezo unaopendwa zaidi duniani.”

Tatizo kubwa
Mario BalotelliHaki miliki ya Mario Balotelli ni mchezaji mwengine maarufu ambaye amewahi kurushiwa maneno ya ubaguzi wa rangi msimu huu
Mashabiki wa Inter Milan walivyojitetea dhidi ya madai ya ubaguzi wa rangi kwa mchezaji wao ilikuwa ni moja ya mifano hai ya ubaguzi wa rangi inayozunguka soka ya Italia kwa sasa.

Mshambuliaji Mario Balotelli wa klabu ya Brescia alisema kwamba mashabiki waliokuwa wanamrushia matamshi ya ubaguzi wa rangi mapema mwezi huu, ” Mawazo yao ni finyu” na ” Wapumbavu”.

Fugazzotto mwenyewe alitaja tukio la Koulibaly msimu uliopita. Mchezaji wa Everton, Moise Kean, alipitia unyanyasaji wa aina hiyo timu yake ilipokuwa anachezea timu ya Juventus wakati inamenyana na Cagliari.

Mwaka 2017, kiungo wa kati wa timu ya Pescara Sulley Muntari alitoka katikati ya mechi baada ya kuanza kurushiwa matamshi ya kibaguzi na mashabiki wa Cagliari – lakini badale yake alipigwa marufuku na mamlaka ya soka kwa sababu hatua yake ya kususia mchezo.

Gazeti kuu nchini humo la michezo Corriere dello liliandika makala iliyipa jina la “Black Friday” kumpa motisha mchezaji mweusi Chris Smalling kwa kuungana tena na aliyekuwa mchezaji mwenza wa Manchester United Romelu Lukaku katika mechi ya AS Roma na Inter Milan mwezi uliopita.

Kwa muktadha huu, inaeleweka kwanini ligi ingetaka kufanya jambo kama hilo.

Lakini ujumbe wa kampeni inayoendelea kuonesha kwamba japo wanafahamu kuhusu ubaguzi wa rangi, haina ufahamu wa kutosha wa kukabiliana na suala hili hasa kwa wachezaji wake wenyewe.
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad