Hakika LiverPool Wamepania Kuchukua UBINGWA Baada ya Kuukosa Miaka 17, Wamtandika Mtu 5



Mabingwa wa Ulaya klabu ya Liverpool wameendelea kuonesha njaa ya kutaka ubingwa wa Ligi kuu ya England ambao wameukosa kwa takribani miaka 30 sasa.

Usiku wa kuamkia leo Desemba 5, 2019, Liverpool wameshinda mchezo wao wa wapinzani wa jadi ambao ni Everton kwa kuwafunga goli 5-2, hivyo kuweka rekodi ya kutofungwa na Everton katika mechi 17 zilizopita, ambapo wameshinda 7 na sare 10.

Kwa upande wa kocha wa Jurgen Klopp ameweka rekodi ya kushinda mechi 100 kati ya 159 alizoiongoza Liverpool kwenye Ligi kuu ya England, akiwa ndio mchezaji aliyefikisha idadi ya mechi 100 za kushinda mapema zaidi kuliko meneja yoyote wa Liverpool katika historia.

Klopp sasa anazidiwa na Jose Mourinho tu ambaye alishinda mechi 100 haraka zaidi kuliko kocha yeyote kwenye Premier League. Alifanya hivyo katika mechi 142 tu.

Pia kwasasa Liverpool haijafungwa katika mechi 32 za Ligi kuu ya England. Wameshinda 27 na sare 5. Mara ya mwisho kufungwa ilikuwa Januari 2019 walipopokea kichapo cha 2-1 kutoka kwa mabingwa wa msimu uliopita Man City. Hii ndio rekodi ndefu zaidi ya kutopoteza mechi kwa Liverpool katika historia yao.

Naye mlinzi wa kulia wa Liverpool Trent Alexander-Arnold ndio mchezaji aliyetoa pasi nyingi za magoli tangu kuanza kwa msimu uliopita 2018/2019 hadi huu wa 2019/20 kwenye ligi kuu ya England. Ametoa Assist 18 huku 15 zikiwa ni mwaka huu.

Divock Origi sasa ni mchezaji wa tatu katika historia ya Liverpool kufunga magoli mengi zaidi dhidi ya Everton. Amefunga matano, akizidiwa na Robbie Fowler mwenye magoli 6 na Steven Gerrard mwenye magoli 9.

Katika mechi nyingi jana, Man United ilishinda 2-1 dhidi ya Tottenham. Na sasa Tottenham imepoteza mechi nyingi zaidi dhidi ya Manchester United kuliko timu nyingine yoyote nchini England. Imepoteza mechi 35.
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad