Magufuli Asaini Sheria ya Watanzania Kujipima VVU Bila Ridhaa ya Mzazi


Dar es Salaam. Waziri wa Afya, Ummy Mwalimu amesema Rais wa Tanzania, John Magufuli amesaini sheria ya Watanzania  kujipima wenyewe Virusi vya Ukimwi (VVU).

Novemba 12, 2019 Bunge la Tanzania lilipitisha marekebisho ya Sheria ya Usimamizi na Udhibiti wa VVU na Ukimwi yaliyoruhusu umri wa kupima virusi vya ugonjwa huo bila ridhaa ya mzazi au mlezi kuwa miaka 15.

Sheria hiyo ilikuwa katika muswada wa Sheria ya Marekebisho Mbalimbali namba saba ya mwaka 2019 uliowasilishwa na kupitishwa na Bunge.

Ummy ameeleza hayo leo Jumamosi Desemba 20, 2019 katika ziara ya kukagua hali ya utoaji wa huduma za afya na ujenzi wa miundombinu ya Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Katavi.

 "Napenda kuwapa habari njema kuwa Bunge la mwezi wa 11 limepitisha sheria na kwa bahati nzuri Rais amekwishasaini kwa hiyo sasa ni rasmi Tanzania mtu kujipima maambukizi ya VVU mwenyewe.”

“Kwa hiyo hivi vitendanishi (vifaa) vitakuwa vinauzwa kwenye maduka, pia kugawiwa bure baadhi ya maeneo kwa sababu wakati mwingine watu wanaona unyanyapaa kwenda kupima wenyewe," amesema Waziri Ummy.


Amesema Serikali imeweka angalizo kuwa kujipima mwenyewe sio majibu ya mwisho, kuwataka wananchi baada ya kujipima kwenda katika vituo vya afya kwa ajili ya kuthibitisha na ushauri zaidi.

Waziri Ummy ameagiza kuendelea kutoa elimu ya afya kwa wananchi, hasa wanaoishi na VVU kutumia dawa kwa usahihi kulingana na maelekezo ya watoa huduma.

Mwananchi
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad