Gigy Money na Mama yake KIMENUKA...Mama Atoa Laana



MAMA wa mwanamuziki wa Bongo Fleva, Gift Stanford ‘Gigy Money’, Fatuma Katunda ‘Kissa’ amemlaani mwanaye huyo na kufikia hatua ya kusema asimzike kutokana na alichomfanyia.


Akizungumza na Risasi Mchanganyiko kwa masikitiko makubwa, mama Gigy alisema hivi karibuni mwanaye huyo alikwenda nyumbani kwake maeneo ya Keko-Akida, Dar na kumporomoshea matusi ya nguoni kisa ugonjwa wa mwanaye, Maryan.


“Alichonifanyia Gigy sitaki hata kumuona, nilikuwa ninaishi na mtoto wake Maryan kutokana na kazi zake kuwa hazitabiriki, sasa Gigy alikuja nyumbani kwangu Keko akamkuta mtoto anaumwa kwa sababu ana pumu ya ngozi.

“Hapo ndipo alipoanza kunitukana matusi ya nguoni akidai kwamba nimeshindwa kumuhudumia mtoto wake vizuri mpaka akaugua.


“Nikamwambia nimeshampeleka hospitali na anatumia dawa, hakutaka kunielewa akaendelea kunitukana. Ikabidi nimwambie simtaki siyo mwanangu maana mtoto anayemjua mama hawezi kumtukana kiasi kile.

“Akanijibu kuwa anatafuta mama mwingine, kwa hiyo yeye atafute huyo mama mwingine na mimi hata nikifa asinizike,” alisema mama Gigy.


Ili kujua mwanamuziki huyo ana lipi la kuzungumza baada ya mama yake kumtolea laana, Risasi Mchanganyiko lilimtafuta Gigy lakini mpaka gazeti hili linakwenda mtamboni, simu yake ya mkononi ilikuwa ikiita tu bila kupokelewa na hata alipotumiwa ujumbe mfupi, nao hakuujibu.


STORI: NEEMA ADRIAN, RISASI

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad