Baada ya Wazazi Wangu Kufariki Boyfriend Analazimisha Tufange Ndoa Harahara Bila ya Harusi...Naombeni Ushauri


ANAOMBA USHAURI : Mimi ni binti wa miaka 29, sijaolewa lakini nina mchumba wangu ambaye tumekaa kwenye mahusiano naye kwa miaka 7 sasa, yeye anafanya kazi ni mwanajeshi lakini ni wale watu ambao hawahudumii kabisa, mimi ni mwalimu na kipato changu ni kidogo kuliko yeye. Amekua ni mtu wa kunilalamikia kila siku, akija akinililia shida nikikataa kumsaidia basi hununa na kuacha kupokea simu zangu hata kwa wiki nzima, mimi hujitrahidi kumtafutia alichoniomba na kumpa, nimekua nikifanya hivyo kwa muda mrefu kila siku nikijariubu kumridhisha yeye tu.

Nimeshaizoea hiyo hali kwani nimeomba Mungu ataabdilika habaidliki. Sababu ya kuja kwenu nikuwa, aktika kipindi chote hicho sual la ndoa limekua gumu sana kwake, kila nikimuambia amekua mtu wa kubaidlika badilika, mara nne alishaniambia kuwa anatuma watu kwetu lakini hatumi, anasingizia sababu nyingine mara kazini hivi, mara nilikua na kile na mambo mengi, nmimekua nikimfumania na wanawake tofauti tofauti lakini namsamehe ingawa hata kuomba msamaha haombi, ananiambia kuwa yeye ni mwanaume hawezi kuwa na mwanamke mmoja.

Sababu ya kuja kwako nikuwa, wmezi uliopita nilifiwa na Mama yangu, kwetu tuko wawili na baada ya Baba kufariki dunia basi Mama ndiyo alikua anasimamia kila kitu. hata arubaini haijaisha mchumba wangu katuma watu eti anataka tufunge ndoa ya harakaharaka hata bila sherehe, mimi nimeshangaa sana kwani bado niko kwenye machungua nasema anataka kufunga ndoa na mimi ili kunifariji katika kipindi hiki kigumu. Nilikubali na kutaka kuongea na baadhi ya ndugu zangu kuwaambia.

Lakini kabla ya kufanya hivyo kuna mwanamke wake mmoja ambaye mara nyingi huwa tunagombana akanitumia meseji za matusi, akiniambia naringia kuolewa lakini sipendwi bali mwanaume anataka mali za urithi tu anampenda yeye. Tulitukanana sana lakini baadaye nimefikiria, kama tukigawana mali ni mimi na mdogo wangu nusu kwa nusu, Mama kaacha nyumba nne magari na vitu vingine vingi, je hivi ni kwelia anvitaka hivyo vitu au ananipenda, nimechanganyikiwa sijui nifenye nini,nawaza kumuuliza lakini naogopa kumuudhi akaacha kunioa, naomba ushauri wenu jamani.
Tags

Post a Comment

1 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Kabla sijatoa Ushauri wangu kwako.
    kwanza jitambulishe.

    ReplyDelete

Top Post Ad

Below Post Ad