Matokeo ya Simba Dhidi ya UD Songa yazidi Kumtesa Mo Dewji


Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa Simba SC, Mohammed Dewji amesema kuwa wana mpango wa kukuza vipaji ili timu hiyo kuja kunufaika hapo baadaye na kufanya vizuri barani Afrika.

Amesema hayo leop katika Mkutano Mkuu wa Klabu ya Simba ulofanyika kwenye Ukumbi wa Mikutano ya Kimataifa ya Mwalimu Julius Nyerere.

"Tuna mpango wa kufungua Simba academy ili hapo badae tuje kuvuna vijana waliolelewa kwenye asili ya Simba. Tuwafundishe vijana hao thamani ya Simba na falsafa ya uchezaji wa Simba, na sambamba upendo ili wawe na uchungu zaidi na klabu yetu.".

"Msimu uliopita ulikuwa mzuri sana kwetu kwa ujumla wake. Kucheza hatua ya Makundi ya Ligi ya Mabingwa barani Afrika na kisha kuvuka hadi robo fainali ilikuwa ni jambo kubwa kwa klabu, ukizingatia pia tuliweza kutetea ubingwa wetu wa nchi.".

"Kuzifunga nyumbani klabu kubwa kama Mbabane, Nkana, Soura, Ahly na AS Vita ilikuwa ni heshima kubwa. Hususani tulikuwa tukiwafunga mbele ya mashabiki wetu 60,000 waliokuwa wakituunga mkono kwa hali na mali. Binafsi msimu uliopita ulikuwa amazing.".

"Niliumia sana kupoteza mechi iliyoandaliwa na wadhamini wetu Sportpesa, ambayo tulicheza na klabu kubwa ya Sevilla kutoka Hispania. Ile mechi tulikuwa tushaongoza kwa idadi nzuri ya magoli, lakini kilichotokea hadi sasa sielewi, lakini ndio football ilivyo".
.
"Tulipata shida kidogo katika msimu huu. Nikisema ni bahati mbaya ni utetezi dhaifu, itoshe kusema yaliyotokea msimu huu kwenye #CAFCL ni fundisho kuu kwetu, na nadhani hatupaswi kurudia makosa tuliyoyafanya. Ilikuwa ni aibu kwetu, na tulijiangusha".

"Binafsi bado sijakaa sawa hadi leo baada ya matokeo ya mechi yetu dhidi ya timu ya UD Songo. Nilikuwa sipo nchini. Baada ya mechi ile kuisha, nililia mnoo.".
.
"Iliniumiza kupita maelezo. Lakini tumefundishwa katika soka kukubali matokeo yote matatu, ingawa mimi nataka klabu hii, iwekeze katika tokeo moja tu, la ushindi! ".

"Mhe mgeni rasmi, mbali ya kutolewa katika #CAFCL, bado sijaridhishwa sana na mwenendo wetu katika ligi ya nyumbani, hata kama tunaongoza ligi. Simba inapaswa icheze kama bingwa mtetezi na kwa soka letu lenye kuburudisha na kutoa matokeo sahihi.".
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad