Mbunge Mdee: Tunachojua Tito yupo mikononi mwa Polisi tunamtaka arudi akiwa hai


Mbunge wa jimbo la Kawe (Chadema), Halima Mdee, amesema jeshi la polisi hata wakanushe vipi wanachokijua ni kuwa Ofisa wa kitengo kutoka Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu (LHRC), Tito Magoti yupo mikononi mwao.

Mdee alisema wanachokitaka na kijana huyo kurejeshwa kwa familia yake akiwa hai.

Kiongozi huyo aliandika ujumbe huo katika ukurasa wake wa Twitter kuwa kauli zenu ya kujichanganya haziwezi kuwasaidia.

“Moto mnauchochea mtashindwa kuuzima,” aliandika Mdee.


Halima James Mdee

Jeshi la POLISI!! Hata mkanushe VIPI, sisi RAIA wa TANZANIA tunajua TITO MAGOTI yupo MIKONONI MWENU!! Tunachotaka Kijana HUYU arejeshwe kwa FAMILIA yake AKIWA HAI!! Kauli zenu za KUJICHANGANYA HAZIWEZI kuwasaidia!!MOTO mnaouchochea mtashindwa KUUZIMA.


Ofisa Tito awali ilisemekana ametekwa Desemba 20 mwaka huu katika eneo la Mwenge baada ya kuchukuliwa na kuingizwa katika gari na watu wasiojulikana.

Baada ya taarifa hizo kueneo mtandaoni kwa wingi, Kamanda wa polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Lazaro Mambosasa, alitoa taarifa kuwa wanamshikilia kwa ajili ya mahojiano bila kueleza yupo kituo gani.

Jana Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kinondoni, Mussa Taibu, akizungumza na waandishi wa habari alisema hana taarifa za kukamatwa kwa Tito licha ya Mambosasa kusema wanamshikilia.
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad