Dawa za Kuzuia MIMBA Baada ya Kujamiiiana zapendekezwa Kuuzwa Katika Madaku ya Kawaida ya Reja Reja

Ripoti mpya iliyotolewa na Chuo kimoja Uingereza cha Madaktari Bingwa wa Afya ya Uzazi cha ‘Royal’, imependekeza vidonge vinavyomezwa ktk hatua ya awali ya kuzuia mimba baada ya Mwanamke kushiriki tendo la ndoa bila ya kutumia kinga vianze kuuzwa maduka ya kawaida kama kondomu.

Ripoti hiyo iliyopewa jina la 'Maslahi Bora kwa Wanawake' inapendekeza Wanawake waruhusiwe kutumia dawa za kuzuia mimba wakiwa majumbani pindi tu wakimaliza kushiriki tendo bila kinga na waruhusiwe pia kutumia dawa, ikithibitika kwamba wana mimba ambayo ipo chini ya Wiki kumi.

Ripoti hiyo mpya ya Chuo cha ‘Royal’ cha Uingereza inasema dawa za kuzuia mimba mara tu baada ya kujamiiana bila kinga,vipimo vya ujauzito na Kondomu vipatikane ktk maduka ya kawaida “Sio lazima Mwanamke afike kwa Mtaalamu inamfanya asiwe huru, ajisikie aibu na hata kuhukumiwa”
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad