Mkwasa: Simba Wepesi tu, Wanafungika



KATIKA kuelekea mchezo wa watani wa jadi, Kaimu Kocha Mkuu wa Yanga, Charles Boniface Mkwasa, ametamba kuwa wapinzani wao Simba ni wa kawaida, hivyo hana hofu mara watakapokutana.

 

Kauli hiyo aliitoa kocha huyo mara baada ya kupata ushindi mnene wa mabao 4-0 walipovaana na Iringa FC juzi kwenye Uwanja wa Uhuru jijini Dar es Salaam.

Simba na Yanga zinatarajiwa kuvaana Januari 4, 2020 mchezo unaotarajiwa kujaa upinzani mkubwa utakaochezwa Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.

 

Akizungumza na Championi Jumatatu, Mkwasa alisema kuwa watani wao Simba anawafahamu, hivyo ni timu ya kawaida ambayo haimpi hofu mara watakapokutana siku hiyo.

Mkwasa alisema hivi sasa ameiweka kando Simba na badala yake akiendelea kukinoa kikosi chake kwa ajili ya michezo mitatu ya Ligi Kuu Bara kabla ya kuwavaa Simba.

 

Aliongeza kuwa anafurahishwa na uimara wa kikosi chake ikiwemo safu yake ya ushambuliaji ambayo juzi kwenye mchezo na Iringa FC walifunga mabao manne tofauti na awali walikuwa wakipata ushindi kiduchu.

 

“Siyo muda muafaka wa kuanza kuuzungumzia mchezo wetu dhidi ya Simba, labda niseme kuwa ni timu ya kawaida inayofungika, hivyo sina hofu mara nitakapokutana nayo.

 

“Nafurahia kuona timu yangu hivi sasa ikitengeneza nafasi za kufunga ambazo wanazitumia vema kwa kuzifunga, ukiwemo mchezo wetu tuliocheza na Iringa FC.

“Licha ya kufunga mabao hayo, bado ninaendelea kuiboresha safu yangu ya ushambuliaji ili ifunge mabao zaidi,” alisema Mkwasa.

 


Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad